Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia imewataka watanzania wote nchini waliopoteza vyeti vyao vya
elimu watoe taarifa mapema katika sehemu husika na wasisubiri mpaka pale
wanapokuwa na uhitaji navyo ndio waanze kuhangaika.
Hayo yameelezwa leo Bungeni na Naibu Waziri Wizara ya hiyo Mhe. William Ole Nasha kwa niaba ya
Waziri ya Waziri Sayansi, Teknolojia wakati alipokuwa anajibu swali
lililoulizwa na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato David Chumi ambapo alitaka
kufahamu serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu ina mpango gani wa
kuwasaidia watanzania waliopoteza vyeti vyao vya elimu na kuvipata vingine.
"Muhitimu aliyepoteza cheti
hupatiwa cheti mbadala au uthibitisho wa matokeo kwa kufuata taratibu
zilizowekwa kama kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi, kutangaza gazetini na
endapo cheti hakikupatikana hata baada ya kukitangaza katika vyombo vya habari
basi muhitimu atahitajika kujaza fomu maalumu",alisema Mhe. William Ole Nasha.
Pamoja na hayo, Mhe. William Ole
Nasha aliendelea kwa kusema "natoa wito kwa wananchi kuwa iwapo
umepoteza cheti cha masomo, anza taratibu za kuomba cheti mbadala, usisubiri
mpaka unapokuwa na uhitaji ndipo uanze taratibu za kuomba".
Kwa upande mwingine, Mhe. William
Ole Nasha amesema muombaji wa cheti mbadala au uthibitisho wa matokeo hupatiwa
huduma baada ya kumaliza utaratibu wote uliyowekwa na Wizara hiyo.
Muhitimu aliyepoteza cheti hupatiwa cheti mbadala.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment