Wananchi zaidi ya
milioni 25 nchini Tanzania wamedaiwa kuwa hawapati huduma za kimahakama
kutokana na upungufu wa majengo ya mahakama na uhaba wa watumishi hususani
kwenye mahakama za mwanzo.
Takwimu hiyo imebainika hapo jana
katika uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo wakati Jaji Mkuu wa
Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alipozindua jengo jipya la kisasa la mahakama ya
wilaya mkoani Pwani.
Jaji Mkuu amesema kwamba kukosekana
kwa huduma za mahakama karibu ndiyo sababu inayopelekea wananchi kukosa huduma
hizo za kisheria, kitendo ambacho kimempelekea kuwataka viongozi wa serikali
katika ngazi za mikoa na wilaya kuona mhimili wa huo kama mdau wa serikali
katika ustawi wa wananchi kwa kusogeza huduma hizo karibu.
Mh. Jaji mkuu , amesema maboresho ya
mahakama yana lengo la kuongeza idadi ya wananchi watakaopata huduma za
mahakama hivyo kujengwa kwa mahakama mpya kutapunguza makali ya uhaba wa
mahakama katika maeneo mengi hapa nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Eng. Everest Ndikilo amesema bado kuna changamoto kubwa za katika
mahakama za mwanzo na kwani majengo yake hutumika pamoja na taasisi nyingine,
jambo linalopelekea kupunguza utulivu katika usikilizaji wa mashauri.
WANANCHI MILIONI 25 HAWAPATI HUDUMA ZA KIMAHAKAMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment