Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kutoa pesa za kitanzania jumla ya
Bilioni 10 Kwa Idara ya Uamiaji nchini ili kuboresha makao makuu ya idara hiyo.
Akizungumza leo katika uzinduzi wa
Pasi za kusafiria za mfumo wa kielektroniki, Rais Magufuli amesema kwamba
ameamua kutoa pesa hizo kutokana na uzalendo unaooneshwa na Idara hiyo.
Rais Magufuli amesema kuwa kutokana
na jinsi idara hiyo inavyojitahidi kufanya kazi kwa juhudi kubwa ndiyo maana
aliamua kuwapatia nyumba 103 mkoani Dodoma ambapo serikali
imewahamishia makazi yake na kuongeza kuwa ni taasisi ya kwanza kupatiwa nyumba
katika mji huo.
"Dkt. Makakala Katafute
eneo, nitawapa bilioni 10 wakati wowote mutakapozihitaji muanze kujenga makao
makuu ya uhamiaji, na natoa hizi kwa shukrani ya kazi nzuri unayofanya wewe na
watendaji wako". Rais Magufuli
Ameongeza "Hapa jinsi
palivyokaa kaa hapafananii na makao makuu ya uhamiaji. Na kwa vile mmekubali
kuhamia Dodoma ni lazima tuwe na jengo zuri litakalokaa kama makao makuu
ya Immigration yenye 'parking nzuri hata mtu akitoka huko anajua kwamba
anakwenda uhamiaji. Najua kuna baadhi ya wafanyakazi watalaumu kuhama kwa sabab
RAISI ATOA BILIONI 10 KWA UHAMIAJI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment