Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Esther Bulaya amesema bado lipo hitaji
muhimu la kuwepo fao la kujitoa kwani linaweza kumtoa mwanachama kwenye
umaskini wa kipato.
Mhe. Ester Bulaya ameeleza hayo leo
Bungeni wakati alipokuwa anatoa maoni ya kambi hiyo baada ya kuwasilishwa
muswada wa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma wa mwaka
2017 ambao umelenga kuunganisha mifuko minne ya umma na kuwa mmoja wa hifadhi
ya jamii kwa watumishi wa umma.
"Bado kuna umuhimu mkubwa wa
kuwa na fao la kujitoa kama ilivyokuwa linatolewa na mifuko iliyokuwapo ni la
msingi na lazima. Kwani mwanachama anakuwa tayari na akiba yake na hivyo huo
unakuwa ni mtaji wa kumtoa kwenye umaskini wa kipato", alisema Bulaya.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama amesema lengo la kuunganishwa kwa mifuko hiyo ya pensheni
ambayo ni PSPF, LAPF, GEPF na PPF ni kukidhi kilio cha muda mrefu cha
wafanyakazi kuhusu kuunganisha mifuko hiyo ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Bulaya"Bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na fao la kujitoa "
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment