Mke wa Mzee Majuto ambaye
anafahamika kwa jina la Aisha Mbwana amefunguka na kuwaomba Watanzania
waendelee kumuombe Mzee Majuto ili aweze kupona maradhi ambayo yanamsumbua na
kusema sasa hivi mumewe amelazwa katika hospitali ya Tumaini.
Akiongea na moja ya chombo cha
habari nchini Aisha amesema kuwa toka jana majira ya saa kumi jioni alipokwenda
kwenye hospitali hiyo ya Tumaini walilazwa kutokana na mume wake kusumbuliwa na
tatizo la tezi dume ambalo limeanza kumsumbua takribani miezi miwili sasa.
"Tumekuja hospitali kuanzia
jana saa kumi jioni na tumelazwa kwani Mzee Majuto anaumwa anasumbuliwa na
tatizo la tezi japo kuwa hayupo 'serious' sana kama ambavyo watu wanafikiria,
napenda kuwaambia Watanzania na mashabiki wa Mzee wazidi kumuombea Mungu kwa
sababu bado tunamuhitaji",
amisema Aisha Mbwana
Kwa upande wake Mzee Majuto akiwa
hospitali hapo ambapo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji aliweza kuongea na kusema
kuwa yeye anazidi kupambana kuhakikisha anatibu ugonjwa huo na kudai kuwa
kuugua ni ibada.
Watanzania waombwa kumuombea Mzee Majuto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment