Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, BAVICHA, Patrick
Ole- Sosopi amekiri kuwa Chama chake kimeamua kurudi kwenye uchaguzi mdogo
haswa wa Kinondoni na Siha kwa kuwa wagundua dawa ya muhuni ni kuwa muhuni
zaidi.
Ole-Sosopi amesema kwamba baada ya kususia uchaguzi ambao uligomewa kupelekwa mbele sasa wagundua kuwa "dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi hivyo ifahamike na iwekwe rekodi kuwa CHADEMA tumerudi na kushiriki na kufanya uchaguzi".
Mbali na hayo Ole-Sosopi ameongeza kuwa hataki chama chake au kingine kisipendelewe bali waachwe wabishane kwa hoja na mwishowe wananchi waachiwe kufanya maamuzi.
CHADEMA walitangaza kugomea uchaguzi mdogo uliofanyika January 13 kwa madai mbalimbali ikiwepo kufanyia hujuma za wazi katika uchaguzi uliofanyika Novemba 26 huku tume ikilalamikiwa kutofanyia kazi malalamiko hayo.
Dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment