Msanii mkongwe wa filamu za bongo,
Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais
Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia
faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.
Mzee Majuto amebainisha hayo muda
mchache alipotembelewa na Rais Magufuli leo katika hospitali aliyolazwa ya
ya Tumaini iliyopo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa
matibabu ya ugonjwa wa tezi dume unaomsumbua kwa kipindi kirefu.
"Mimi ndiyo mtu wa kwanza
kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli. Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu
bwana, tumepata Rais sio masihara watu wote sasa hivi wana adabu zao wanajua
nini maana ya kazi ukisema jambo watu wanatekeleza, wezi wanakamatwa, wala
rushwa wanakamatwa, wenye vyeti feki hata kama amefanya kazi miaka 20 fukuza,
hii safi", alisema Majuto.
Pamoja na hayo, Mzee Majuto
aliendelea kwa kusema "sisi wazee tunafarijika sasa hivi,
viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui
kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha
ya kupata viongozi wenye msimamo".
Kwa upande mwingine, Mzee Majuto
amesema kupata sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara
kama Dkt. John Magufuli.
MZEE MAJUTO"NILITABIRI RAISI MAGUFULI ATAKUJA"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment