Mbunge Nape Nnauye leo
Bungeni ameipa changamoto Serikali juu ya gharama za kuunganisha umeme na
kuishauri kuendelea kuchaji elfu 27,000 hata baada ya mradi REA kupita
ambapo wataanza kuchaji 177,000 kuunganisha umeme.
Nape Nnauye ametoa ushauri huo
alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwenda kwenye Wizara ya
Nishati
"Kwanza niipongeze Serikali
chini ya Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri wanayofanya ya usambazaji mzuri wa
umeme vijijini hasa REA awamu ya 3, kwa kuwa gharama za kuunganisha umeme
wakati mradi unaendelea ni elfu 27,000 na mradi ukipita ni 177,000 na kwa kuwa
idadi kubwa na nzuri ya watumiaji wa umeme ni biashara nzuri kwa TANESCO
kwanini bei hii isiwe moja ya elfu 27" alisema Nape Nnauye
Hata hivyo Nape Nnauye aliendelea
kusisitiza kuwa kama jambo hilo halitawezekana basi REA waendelee na uwekaji wa
nguzo na miundombinu na TANESCO wafanye kazi moja ya kupeleka umeme na
kukusanya kodi baada ya kupeleka umeme.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati
alijibu hoja hiyo na kudai kuwa amepokea ushauri huo wa Mbunge wa Mtama na kuwa
atapeleka katika ngazi zingine na kuona Serikali nini itafanya
"Wazo alilosema Kaka yangu Nape
Nnauye linapokelewa na litafanyiwa kazi kwani ni la msingi kwa sababu Wizara
yetu na shirika letu la TANESCO na wadau wengine wa nishati tunauza bidhaa hii
hivyo ni vema tunapouza tupate wateja wengi ili tupate mapato na kuendesha
shughuli mbalimbali na uwekezaji mpya wa maeneoya nishati"
Nape Nnauye aipa changamoto Serikal
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment