Rais Amtembelea King Majuto Hospitali



Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth leo wamemtembelea mchekeshaji maarufu nchini, King Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili akipatiwa matibabu ya tezi dume.

Mbali na Mzee Majuto ambaye jina lake halisi ni Amri Athuman, Rais Magufuli amewajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali hiyo kuanzia wodi namba tatu mpaka nane.

Mzee majuto aliyejipatia umaarufu maigizo ya ucheshi amemshukuru Rais Magufuli na kumpongeza kwa kusimamia sekta ya afya kwani ameshuhudia huduma nzuri katika hospitali hiyo tangu alipolazwa

“Hatua anazochukua Rais Magufuli zimerejesha nidhamu na uchapakazi, tangu nimefika hapa nimehudumiwa vizuri naamini nitapona haraka na kurejea katika ujenzi wa Taifa,” amesema.

Majuto amemuombea Rais Magufuli aendelee kutekeleza majukumu yake ya kuongoza nchi vizuri, na amebainisha kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali  zimerejesha nidhamu, zimeongeza uchapakazi, zimesaidia kukabiliana na wizi na zimeongeza heshima ya nchi.
Rais Amtembelea King Majuto Hospitali Rais Amtembelea King Majuto Hospitali Reviewed by KUSAGANEWS on January 31, 2018 Rating: 5

No comments: