Wakizungumza baadhi ya walimu
akiwemo Mwalimu wa Somo la Kemia ambaye pia ni Mwalimu wa Nidhamu katika Shule
hiyo, Neema Kimani, Mwalimu Msaidizi wa Taaluma Reginald Chiwangu bidii na
kumtanguliza Mungu ndio siri ya mafanikio hayo.
''Kumtanguliza Mungu kwa kila jambo,
bidii ya walimu na wanafunzi, utawala bora na kusikiliza ushauri kutoka kwa
wadau mbalimbali wa elimu ndio vimechangia shule yetu kuongoza kitaifa'',
wamesema.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
nne shuleni hapo akiwemo Joyce Msigala, Lorette Leone na Bibiana Karumuna wamesema
kuwa matokeo hayo yametoa mwanga wa jinsi gani walijiandaa ili kufanya
vizuri kwenye mtihani wao.
Wahitimu wa Shule ya Sekondari ya
wasichana ya St. Francis waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ambao ndio
wameongoza kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza walikuwa 92.
Baada ya shule ya Sekondari ya wasichana ya St. Francis Mjini Mbeya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana wameeleza kuwa bidii ya walimu na wanafunzi ndio siri ya mafanikio hayo.
Siri ya Kufaulu ni Kumtanguliza Mungu kwa kila jambo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment