Kampeni za uchaguzi wa ubunge zikiwa bado zinaendelea katika
majimbo ya Kinondoni, Siha na kata 10, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi amevikumbusha vyama 12 vinavyoshiriki uchaguzi utakaofanyika februari
17, 2018 kuendesha uchaguzi huo bila kuvunja sheria za nchi.
”Natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi
ndogo za ubunge na udiwani zinazoendelea katika majimbo na kata. Hivyo natumia
fursa hii pia kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi” amesema
Jaji Mutungi.
Aidha ameviasa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kuheshimu na
kufuata sheria ya vyama vya siasa, sheria ya gharama za uchaguzi na kanuni
zake, kwa kuepuka vitendo vya fujo na lugha za matusi na uchochezi .
Pia Jaji Mutungi ametoa wito kwa wanachama wa chama chochote cha
siasa au kinachoshiriki uchaguzi kutoa taarifa katika mamlaka husika kuliko
kujichukulia sheria mkononi.
Mutungi aingilia kati kampeni za uchaguzi Siha, Kinondoni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment