Mbunge wa Ruaraka Tom J Kajwang’,
ambaye alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga
kwenye viwanja vya Uhuru Park Jumanne amekamatwa.
Mbunge huyo amekamatwa leo
Jumatano mchana na maofisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare nje ya
Mahakama ya Milimani jijini Nairobi.
Alikamatwa muda mfupi baada ya
kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi
wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho.
Kajwang’ na mwanasheria mwingine
Miguna Miguna, ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa matukio ya kwenye viwanja
vya Uhuru Park yaliyomalizikia kwa “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa watu’.
Wakati wa sherehe za kiapo
Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi na alishangiliwa sana na wafuasi wa
Nasa.
Odinga alikula “kiapo” huku
Kajwang’ akiwa amesimama nyuma yake japokuwa wajibu wake katika tukio hilo
bado haujafahamika
|
|
ALIYEMUAPISHA RAILA ANASWA NA POLISI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment