JUMUIYA YA WAZAZI ARUMERU WADHIMISHA MIAKA 41 KWA KUTOA MSAADA HOSPITALI YA SELIANI NA KUPANDA MITI ,
Akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa wilaya
hiyo Bwana Jastini Lengitae amesema kuwa wao kama jumuiya ya wazazi wana jukumu
kubwa la kuhakikisha wanasimamia vizuri jumuiya hiyo kwa kutoa misaada pamoja
na kusimamia nidhamu kwenye za jamii
Pia mwenyekiti huyo amesisitiza suala la nidhamu kwa
wanafunzi katika shule hiyo ya Mringa Sekondari na kuwataka wazazi na walimu kusimamia nidhamu ya wanafunzi ili kuwa ni kizazi ambacho ni bora kwa siku za mbeleni.
Kwa upande katibu wa Wazazi wa wilaya hiyo Bi Rehema
Mohamed amesema kuwa wamefanya kwa jinsi walivyoweza kwa kuwa kutoa ni moyo
hivyo wameona washiriki pamoja katika hospitali ya Selian.
Hata hivyo katibu wa hospitali ya Selian Ngaramtoni
Bwana Peter Ngurumwa ameshukuru jumuiya ya wazazi kwa kufanya zoezi hilo ambalo
ameomba wengine kuiga mfano wa jumuiya hiyo.
Naye Fransisca kivuyo muuguzi wa zamu katika wodi ya
watoto amesema kuwa wameurahia ujio wa jumuiya hiyo pamoja na kuwasisitiza
wengine kufanya hivyo kwa ni moja ya ibada
JUMUIYA YA WAZAZI ARUMERU WADHIMISHA MIAKA 41 KWA KUTOA MSAADA HOSPITALI YA SELIANI NA KUPANDA MITI ,
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment