AUWAWA KWA KUCHUNWA NGOZI KAMA MNYAMA NA KUNYOFOLEWA VIUNGO

Mzee mmoja aliyetambulia kwa majina ya Tuntinala Kunyepa (75) mkazi wa Kijiji cha Ihanda Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, amekutwa akiwa ameuawa na kuchunwa ngozi na kisha kutolewa baadhi ya viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana .

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, Yusuph Sarungi, amesema, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana.

Kamanda Yusuph amesema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hiilo huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina ambapo uchunguzi na msako mkali unaendelea kuwabaini waliohusika .


AUWAWA KWA KUCHUNWA NGOZI KAMA MNYAMA NA KUNYOFOLEWA VIUNGO AUWAWA KWA KUCHUNWA NGOZI KAMA MNYAMA NA KUNYOFOLEWA  VIUNGO Reviewed by KUSAGANEWS on January 31, 2018 Rating: 5

No comments: