Madiwani watatu wa
CHADEMA halmashauri ya Mji wa Njombe wametolewa nje ya kikao cha baraza la
madiwani na kusimamishwa kuhudhuria vikao 3 kutokana na kujadili mkataba wa
halmashauri na kampuni iliyowekwa kukusanya ushuru ambayo inawanyanyasa
wananchi
Madiwani hao ni pamoja na George
Sanga diwani Kata Ramadhani, Sigrada Mligo, diwani viti maalum, Legnard Danda,
diwani kata Ihungilo ambao walitolewa kwenye mkutano na kusimamishwa kuhudhuria
vikao vitatu baada ya kuhoji mkataba wa halmashauri na kampuni ya Ihagara inayo
kusanya ushuru mjini Njombe ambayo inadaiwa kuwanyanyasa wananchi.
Awali Mwenyekiti wa halmashauri ya
Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alipiga marufuku kujadili suala hilo kwa madai
kuwa baraza halina mkataba huo na hakuna palipo andikwa jina la kampuni hiyo.
"Ihagala kama nani? Tumewaambia
sisi hatujamwajiri na baraza hili halijamwajiri huyo Ihagala hivyo sisi
tunamjadili kama nani? Nimewaambia hayo mapendekezo yote wayapeleke kwa
Mkurugenzi yeye ndiye mwajiri wa Ihagala" alisema Mwanzinga
MADIWANI WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VITATU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment