Makamu wa Rais wa zamani
wa Kenya ambaye sasa ni kiongozi mwenza wa NASA, Stephen Kalonzo Musyoka nyumba
yake imepigwa bomu usiku wa kuamkia leo katika eneo la Karen, Nairobi Kenya na
watu wasiojulikana.
Maafisa wa polisi nchini Kenya
wamezingira makazi ya kiongozi huyo leo mapema baada ya usiku watu
wasiojulikana kurusha bomu la mkono na kufyatua risasi katika nyumba hiyo.
Hata hivyo taarifa kutoka nchini
Kenya zinasema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha na polisi wamesema
watatoa taarifa kamili baada ya kukamilisha uchunguzi wao kufuatia tukio hilo.
Kalonzo Musyoka jana Januari 30,
2018 alishindwa kutokea kwenye sherehe za kujiapisha kwa kiongozi Mkuu wa
upinzani nchini Kenya Bwana Raila Odinga kuwa Rais wa wananchi wa Kenya sherehe
zilizofanyika bustani ya Uhuru jijini Nairobi.
Nyumba Kiongozi wa NASA yapigwa Bomu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment