Hapo Jana kiongozi wa
muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, Raila Amolo Odinga, amejiapisha
kuwa Rais wa watu wa Kenya, jambo ambalo limeleta hali ya sintofahamu kwa watu
wengi waliokuwa wakifuatilia suala hilo.
Kitendo hicho cha Raila Odinga
kujiapisha kinaibua maswali nini kitafuata, baada ya kuonekana kufanya kosa
kisheria, huku wengine wakisema kuwa hana kosa kisheria kwani hajajiapisha kama
Rais wa Kenya, isipokuwa ni Rais wa watu.
Maneno yaliyotamkwa kwenye kiapo
hiccho yanasema kwamba ..."Mimi, Raila Amolo Odinga, kwa kutambua wito wa
juu kuchukua madaraka ya Rais wa Watu wa Jamhuri ya Kenya, naapa kuwa nitakuwa
mwaminifu na kuwa na utii wa kweli kwa watu na Jamhuri ya Kenya, kwamba
nitahifadhi, kulinda na kulinda Katiba ya Kenya, kama ilivyowekwa na sheria na
sheria nyingine zote za Jamhuri kama ilivyopitishwa na Watu wa Kenya;
Nitawalinda na kuendeleza uhuru na heshima ya Watu wa Kenya.
Basi nisaidie Mungu",
yalisikika maneno haya yakitamkwa kinywani mwa Odinga.
Tukio hilo lilihudhuruwa na maelfu
ya Wakenya kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo, huku baadhi ya viongozi
wengine wa Nasa ambao nao walitakiwa kuwa miongoni mwa wanaoapa kuikacha na
kuingia mitini, akiwemo Kalonzo Musyoka na Mudavadi.
Baada ya hapo Raila Odinga
alibadilisha status yake ya twitter na kuweka kama Rais wa Kenya, lakini
baadaye alibailisha na kuweka kama Rais wa watu.
Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mtu
ambaye ataapa kuwa Rais wakati bado kuna Rias mwengine madarakani aliyewekwa
kisheria na katiba ya nchi hiyo, anafanya kosa la uhaini ambalo hukumu yake ni
kunyongwa.
Mpaka sasa serikali ya Kenya
haijatoa tamko lolote juu ya kitendo hicho cha Raila Odinga, ambacho watu wengi
wana shauku ya kutaka kujua nini kitafuata? Je, atashtakiwa au ataachwa huru!?
Alichokisema Odinga kwenye kiapo chake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment