Magaidi wahukumiwa miezi 6 kwa kuvua Nguo mahakamani

Watuhumiwa 24 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi za ugaidi jijini Arusha wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuvua nguo na kisha kugoma kuingia ndani ya chumba cha Mahakama kusikiliza kesi zinazowakabili.

Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Nestory Baro, ambapo amesema, watu hao wamehukumiwa kwa mujibu wa kifungu namba 114 (a) cha mwongozo wa mashtaka ya jinai.

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo baadhi ya watuhumiwa walivua nguo zao na kubakisha nguo zao za ndani wakati wakipandishwa kwenye karandinga kurejeshwa katika gereza kuu la mkoa wa Arusha.

Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Serikali ,Augustino Kombe aliiomba Mahakama hiyo iwachukulie hatua kali na kutoa adhabu kwa watuhumiwa wa kesi hizo wanaogoma Mahakamani.
Magaidi wahukumiwa miezi 6 kwa kuvua Nguo mahakamani Magaidi wahukumiwa miezi 6 kwa kuvua Nguo mahakamani Reviewed by KUSAGANEWS on January 30, 2018 Rating: 5

No comments: