Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kuunga mkono agizo la Rais John
Magufuli la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kununua bidhaa
zinazozalishwa nchini.
Akizungumza leo,Mwijage
amesema manunuzi ya vifaa kutoka nje kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
taasisi za Serikali, kuacha kununua vinavyotengenezwa nchi ni kwenda kinyume na
agizo la Rais.
Lazima hizi taasisi kuonyesha uzalendo wao kwa kununua
bidhaa za ndani zenye ubora, kwanza watawezesha viwanda kufanya kazi lakini pia
wataongeza pato la taifa na ajira kwa watanzania,” amesema Mwijage.
Amesema Serikali inafuatilia michakato ya zabuni mbalimbali,
kuona kama inakwenda sambamba na maagizo ya Serikali, kwamba uzalendo wa
watendaji wa taasisi hizo pia utapimwa kwa kutekeleza maagizo ya serikali.
Hili ni suala ambalo lazima tushirikiane ni zaidi ya
uzalendo kwani kama kuna bidhaa zenye viwango zinazalishwa nchini, kwanini
taasisi yako katika miradi yake ikanunuwe vifaa nje,"amehoji.
WAZIRI MWIJAGE AUNGA MKONO AGIZO LA RAISI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment