Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Mara kumkamata na kumuhoji meneja
wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wa mkoa wa Mara, mhandisi Peter
Salim.
Amesema mhandisi huyo anakamatwa kutokana na kushindwa
kutekeleza ujenzi wa mradi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama
Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza
kuwa Serikali ilitoa Sh600 milioni, Aprili, 2017 kwa ajili ya kuanza kwa
ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo, lakini hadi sasa wakala huo
hajafanya kazi yoyote.
Imesema kwa maelezo yake, mhandisi Salim amesema ujenzi wa
ofisi hiyo hadi kukamilika utagharimu Sh3bilioni, kati ya Sh600milioni
zilizotolewa na Serikali Sh400milioni zimetumika kujengea msingi, kauli
iliyopingwa na mkuu wa wilaya hiyo, Anna-Rose Nyamubi.
Waziri mkuu siyo kweli kwamba kuna kazi inayoendelea bali
kilichopo pale ni mashimo ambayo hayajulikani ni ya nini. Pia kuna jengo moja
lilijengwa kwa mabati kama stoo na hakuna mafundi wanaoendelea na kazi,”
amesema Nyamubi.
Pia, Waziri Majaliwa amemuagiza kaimu katibu tawala wa mkoa
wa Mara, Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi
maalumu katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Butiama.
Amesema halmashauri hiyo imekuwa na tabia ya kutumia fedha
za miradi mbalimbali ya maendeleo zinazotolewa na Serikali katika shughuli
nyingine jambo ambalo ni kinyume cha Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Januari
20, 2018 wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri ya wilaya
ya Bitiama.
Pia, aliagiza kuchunguzwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Butiama, Solomon Ngiliule pamoja na mweka hazina wa halmashauri hiyo,
Masanja Sabuni na ofisa manunuzi, Robert Makendo.
Amesema viongozi hao wanatakiwa wachunguzwe kutokana na
matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali
zikiwemo Sh12milioni walizotumia kuandaa taarifa ya halmashauri hiyo
Amesema fedha nyingine ni Sh70milioni za elimu maalumu,
Sh288milioni za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazijulikani
zimetumikaje
“Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi fanyeni uchunguzi na naomba
taarifa yake mara mtakapokamilisha,” amesema
WAZIRI MKUU AMURU MENEJA WA TBA KUKAMATWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment