Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa siku 14 kwa
uongozi wa kiwanda cha saruji cha Dangonte mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na
wachimbaji wadogo wa gypsum
Biteko ametoa kauli hiyo leo baada ya
kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na viongozi wake
Amesema mikataba hiyo inapaswa kuwa na kipengele cha
kuwalipa ndani ya siku 30 baada ya kiwanda kukusanya gypsum kutoka kwa
wachimbaji hao, lengo likiwa ni kuleta ufanisi na tija katika biashara zao
“Nimekubaliana hapa kamishna wa kanda atasimamia hili la
mikataba kati ya kiwanda na wachimbaji wa gypsum. Sehemu ya malipo itakuwa
ndani ya mkataba na watalipa ndani ya siku 30,” amesema
Amesema wachimbaji hao wamekuwa wakilalamikia kucheleweshewa
malipo yao baada ya kupeleka kiwandani bidhaa zao.
Nimeambiwa wachimbaji hawa walikuwa wanalipwa baada ya miezi
mitatu lakini kwa mkataba huu ambao wataingia na kiwanda sasa watakuwa
wanalipwa ndani ya siku 30,” amesema Biteko.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuwasaidia
wachimbaji wadogo sambamba na wawekezaji ambao wanapaswa kufanya kazi bila
kusumbuliwa.
“Uwepo wa kiwanda hiki unawasaidia wachimbaji wetu waweze
kupata bei nzuri pamoja na kupata soko la uhakika la kuuza bidhaa zao. Dangonte
wameniahidi kwamba ndani ya muda mfupi watatekeleza agizo hili,” amesema
Biteko amesema lengo la ziara yake ni kuwasaidia wachimbaji
wa gypsum ambao hawana mikataba na kujikuta wakibanwa katika uuzaji wa bidhaa
zao
WAZIRI ATOA SIKU 14 KWA KIWANDA CHA DANGOTE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment