Chama cha ACT-Wazalendo kimesema hakitashiriki uchaguzi
katika majimbo ya Kinondoni na Siha kwa kuwa sababu zilizowafanya wasusie
uchaguzi mdogo uliopita, bado hazijafanyiwa kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho-Bara, Msafiri Mtemelwa amesema changamoto walizozilalamikia katika
uchaguzi wa Januari 13 katika majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini na
Longido bado hazijafanyiwa kazi.
Amesema bado chama hicho kitaendelea kushinikiza Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanya mageuzi katika mchakato wa uchaguzi.
Amesema malalamiko ya chama hicho kwa NEC ni matumizi ya
nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia
chama tawala CCM.
Uchaguzi wa Siha na Kinondoni unafanyika baada ya waliokuwa
wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM Desemba mwaka jana.
ACT WASUSIA UCHAGUZI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment