Kamanda Muslim amesema askari wa usalama barabarani
wanatakiwa kuangalia makosa hatarishi yanayoweza kusababisha kutokea kwa ajali
na kuachana na yale yasiyokuwa ya msingi.
Juzi, Kamanda Mambosasa aliwataka askari hususan wa usalama
barabarani kutumia busara katika utendaji kazi wao ili kuondoa malalamiko ya
uonevu na kuwakandamiza raia na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili
ya kulinda raia na mali zao na kusimamia sheria.
Akizungumza Kamanda Muslim alisema askari
wote wa kikosi hicho wanaelekezwa kuzingatia makosa hatarishi kwa kuwa kazi
kubwa ya kikosi hicho ni kuhakikisha sheria za barabarani zinazingatiwa ili
kupunguza ajali zinazogharimu maisha ya watu
Alisema kuna makosa ambayo hayana athari kulingana na
mazingira husika hivyo askari hawana sababu ya kuyapa kipaumbele
“Naungana kabisa na Mambosasa ila mimi nisitumie neno busara
labda niseme askari wakamate makosa hatarishi, mnamkamata vipi dereva kwa kosa
la taa mchana au wiper mbovu wakati wa jua kali? Hayo yote hayawezi kusababisha
ajali kwa nyakati hizo. Hapo ndipo linapokuja suala na mazingira, wiper zinatakiwa
kufanya kazi kipindi cha mvua
Kuhusu askari wa usalama barabarani kumsimamisha dereva na
kuanza kutafuta kosa, Kamanda Muslim alisema ni muhimu kwa madereva kuzingatia
sheria si muda wote wanasimamishwa kwa sababu ya makosa.
Tatizo ni kwamba madereva wenyewe wameshajenga mtazamo hasi,
sio kila wakati askari anapokusimamisha lazima uwe na kosa inawezekana anataka
kukupa tahadhari huko unakoelekea sio kuzuri hivyo uongeze umakini.
“Ninachosisitiza madereva wafuate sheria, waache kulalamika.
Wakizingatia sheria sidhani kama hao askari watakuwa wanawasimamisha ovyo kama
wanavyodai,” alisema Kamanda Muslim.
Pia aliungana na Mambosasa kuwataka madereva wasikubali
kutoa fedha kwa askari bila kupata risiti zinazotokana na mashine au fomu namba
101 ya polisi inayofahamika kama ‘notification’.
Kadhalika alisema askari wa pikipiki maarufu kama tigo
wataendelea kufanya kazi yao ya kuzuia uhalifu unaohusisha makosa ya jinai na
usalama barabarani na kusisitiza kuwa hawana mamlaka ya kutoza faini Ukusanyaji
wa mapato
Kamanda Muslim alionyesha kukerwa na watu wanaohusisha tozo
zinazotokana na makosa ya barabarani na ukusanyaji wa mapato.
Alisema kazi ya kukusanya mapato inafanywa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) tofauti na tozo zinazokusanywa na kikosi hicho kutokana
na uvunjifu wa sheria barabarani.
“Nashangaa wanaosema tunakusanya mapato kwani Jeshi la
Polisi lina biashara gani? Sisi tunatoza tozo zinazotokana na makosa ya
barabarani na lengo letu ni kuzuia ajali na kuhakikisha usalama unakuwa wa
kutosha katika barabara zetu
Tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria na anayepaswa kulipa ni
yule aliyevunja sheria na inasimama badala ya kifungo kwa hiyo watu wanapaswa
kutambua askari wa usalama barabarani hawakusanyi mapato.” Hali ya usalama
barabarani
Kamanda hiyo alisema hali ya usalama barabarani nchini
imeimarika na ajali zinaendelea kupungua kwa kiasi kikubwa.
Alisema hiyo inatokana na askari wa kikosi hicho kuimarisha
ukaguzi na usimamizi wa sheria.
Nikitolea mfano wa leo (jana) yaani ndani ya saa 24, nchi
nzima kuna ajali tatu pekee. Hii ni hatua kubwa na siku nyingine hakuna ajali
kabisa hayo ni matokeo ya usimamizi wa sheria kazi inayofanywa vizuri kabisa na
askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Usimamizi wa sheria umeongezwa maradufu kwenye maeneo ya
kuvukia watembea kwa miguu, nimesisitiza lazima dereva asimame aangalie pande
zote ndipo apite hata kama hakuna mtu anayevuka. Kwa magari yanayosafiri
ukaguzi unafanyika kabla hayajatoka vituoni na madereva tunawapima ulevi, huko
njiani askari nao wanajipanga vizuri.”
Kamanda Muslim alisema jitihada zote hizo zinafanyika
kuhakikisha ajali zinapungua au kutokomezwa kabisa.
Alisema, “Hatuwezi kuvumilia watu wapoteze maisha sababu ya
madereva wazembe, hatutafungua ‘tuition’ barabarani ya kutoa elimu.
Kama unataka elimu acha gari lako nyumbani ukija nalo
barabarani na ukavunja sheria neno ni moja tu “kamata” na watalipa faini na
wale ambao watakuwa wagumu zaidi kuelewa neno lao ni “funga” hawa tutawafungia
leseni zao.”
KAMANDA MUSILIMU AUNGA MKONO KAULI YA MAMBOSASA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment