Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia
amewaomba radhi wanachama wa chama hicho tawala kwa ushindi wa kishindo
alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiwa CUF.
Mtulia ametoa kauli hiyo leo Januari 21, mwaka 2018 wakati
akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho wilaya ya Kinondoni.
Mwaka 2015, Mtulia alishinda ubunge wa Kinondoni kwa tiketi
ya CUF, lakini Desemba 2 mwaka jana alijivua uanachama wa chama hicho na
kuhamia CCM, hivyo kupoteza sifa ya ubunge. Hata hivyo CCM kilimpitisha
kugombea ubunge katika jimbo hilo
MTULIA AOMBA RADHI KWA WATU WA KINONDONI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment