Askofu Gwajima apata pigo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Januari 21, 2018 amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi Ruth Basondole Gwajima ambaye amefariki asubuhi ya leo.

Gwajima amesema kuwa mama yake mzazi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 na kuwa mazishi ya mama yake mpendwa yatafanyika siku ya Alhamisi ya Januari 25, 2018 Salasala jijini Dar es Salaama.

"Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018; Salasala Dar es Salaam" alisema Gwajima.
CHANZO EATV

Askofu Gwajima apata pigo. Askofu Gwajima apata pigo. Reviewed by KUSAGANEWS on January 21, 2018 Rating: 5

No comments: