WAZIRI KIGWANGALA ATOA SIKU 7 WATU 4 KUKAMATWA.



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa watu wanne wanaotumiwa kuhusika na matukio ya ujangili la sivyo atakwenda kushtaki kwa amiri jeshi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Dk Kigwangala amesema polisi wana taarifa zote kuhusiana na watu hao kuhusika katika ujangili  pamoja na kula njama ya mauaji ya raia wa kigeni lakini polisi wamekuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua kuhusiana na watu hao.

Amesema kuwa tayari amewasiliana na Jeshi la Polisi kuhusiana na jambo hilo lakini uchukuaji wa hatua hizo umekuwa taratibu.

Pia, Dk Kigwangalla ametoa siku saba kwa wakurugenzi wa makampuni ya uwindaji na ofisa mmoja wa Tanapa kufika katika kikosi maalum ya atakachokiunda kukutana nao kwa mahojiano kuhusu tuhuma mbalimbali.
WAZIRI KIGWANGALA ATOA SIKU 7 WATU 4 KUKAMATWA. WAZIRI KIGWANGALA ATOA SIKU 7 WATU 4 KUKAMATWA. Reviewed by KUSAGANEWS on January 25, 2018 Rating: 5

No comments: