Dar es Salaam. Serikali imeagiza mamlaka zinazohusika na
ubomoaji wa jengo la Tanesco kukamilisha ifikapo Februari mosi.
Akizungumza leo Januari 29 katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa njia za juu katika makutano ya Ubungo na ubomoaji wa ofisi za Serikali ikiwemo la Wizara ya Maji na Tanesco Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kwa upande wa jengo la Wizara ya maji zoezi limekamilika.
"Kama inavyoonekana hapa jengo la maji limekamilika lakini kwa upande wa Tanesco tumeagiza kukamilika Februari mosi hata hivyo nimeona ubomoaji upo kwenye hatua za mwisho" amesema.
Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji Tanesco Khalid James amesema kuchelewa kubomolewa jengo hilo kumetokana na ukosefu wa vifaa maalum vya kubomolea.
Amesema pamoja na kutokuwepo kwa vifaa hivyo, ubomoaji unaendelea hadi Februari mosi ubomoaji utakamilika.
"Kuna vifaa maalum kwa ajili ya kubomolea hivyo hatuna na ndiyo maana zoezi hili linachelewa, lakini ukitaka kujua kwa undani kuhusu hivyo vifaa waulize Mamlaka ya Majengo Tanzania (TBA)"amesema.
Akizungumzia kuhusu gharama za ubomoaji wa jengo hilo na rasilimali nyingine za shirika hilo James amesema inakadiriwa kufikia kiasi cha Sh 700milioni.
Akielezea wapi wataelekea baada ya jengo hilo kubomolewa amesema kwa sasa shirika hilo linahamishia ofisi zake makao makuu ya nchi na kwamba maandalizi yanaendelea.
Hapa hakuna jinsi, kinachofuata ni kwenda makao makuu ya nchi tayari maeneo tunayo Dodoma na maandalizi yanaendelea.

Sumaye: wanaojiuzulu nafasi zao hawatambui majukumu yao
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment