Jaji Mkuu amezindua Kituo cha mafunzo na habari



Dar es Salaam. Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amezindua kituo cha mafunzo na habari za Mahakama ili kuwajengea uwezo watumishi.

Akizindua kituo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Januari 29,2018 Profesa Juma amesema malengo ni kuhakikisha haki inawafikia wananchi kwa wakati na kwa urahisi zaidi.

Amesema kituo hicho kimejengwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.

Jaji mkuu amesema wanawajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwa sababu kuna mambo mengine hawakusoma wakiwa chuoni.

Profesa Juma amesema Tehama inarahisisha kazi kwa kutoa haki kwa wakati na kwa urahisi, pia kuwafikia wananchi.

Amesema maeneo mapya yanayotakiwa kufanyiwa kazi na watumishi wa Mahakama ni makosa ya mtandao, yanayotokana na miamala ya simu na dawa za kulevya.

Jaji mkuu amesema mahakimu na waendesha mashtaka wakipata mafunzo watakuwa na uelewa mmoja katika kutoa haki.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird akizungumzia mfumo huo wa Tehama amesema utasaidia kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi na watapata haki kwa wakati.
Jaji Mkuu amezindua Kituo cha mafunzo na habari Jaji Mkuu amezindua Kituo cha mafunzo na habari Reviewed by KUSAGANEWS on January 29, 2018 Rating: 5

No comments: