Dar es Salaam. Serikali imeanza uhakiki wa walimu wenye
Shahada ya Uzamili ya Elimu wanaofundisha shule za msingi.
Uhakiki huo ulioanza Januari 22,2018 unatakiwa kukamilika Januari 31,2018 na unasimamiwa na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Akizungumza Katibu Mkuu- Tamisemi, mhandisi Mussa Iyombe amesema uhakiki huo unalenga kupata idadi ya walimu wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu waliopo shule za msingi ili kuwa na taarifa zao na watakapohitajika sekondari wapelekwe.
“Tunataka tupate idadi kamili ya walimu wenye masters (Shahada ya Uzamili) ambao wapo shule za msingi,” amesema Iyombe.
Maelezo ya Iyombe yanatokana na barua yake ya Januari 22 aliyoitoa kwenda kwa makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara iliyokuwa na kichwa cha habari ‘orodha ya walimu wenye shahada ya uzamili ya elimu wanaofundisha shule za msingi.”
Katika barua hiyo, Iyombe anasema “Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu. Ofisi ya Rais -Tamisemi inafanya zoezi la ukusanyaji wa taarifa muhimu za walimu wote wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu waliopo katika shule za msingi.”
“Kwa barua hii, mnaombwa kuwataka wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ndani ya mikoa yenu kukamilisha taarifa za walimu hao kwa kuzingatia muundo (template) wa kukusanyia taarifa hii (umeambatishwa).”
Iyombe ametaka taarifa hizo ziwasilishwe Ofisi ya Rais- Tamisemi kabla au ifikapo Januari 31.

Serikali yaanza uhakiki wa Walimu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment