Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Salum Henjewele maarufu 'Scorpion’ aliyekuwa akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho, kwenda jela miaka saba na kulipa fidia ya shilingi milioni 30 kwa kosa la kujeruhi na wizi.
Baada
ya mahakama kumkuta na hatia Salum Henjewele na kufungwa miaka saba ikiwa
pamoja na kulipa fidia ya milioni 30, Saidi Mrisho ambaye alifanyiwa tukio hilo
la kinyama amefunguka na kusema kuwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama
hiyo.
Said Mrisho, mwaka juzi 2016 mwezi Septemba, akiwa maeneo ya Buguruni Kwamnyamani majira ya usiku alivamiwa, akaporwa vitu, akajeruhiwa tumboni na kutobolewa macho yake yote mawili yalipelekea kupatwa na upofu na kutoona kabisaa.
'Scorpion' mtoa macho afungwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment