Rais John
Magufuli amemtumia rambirambi Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma kutokana na
kifo cha Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Robert Kisanga.
Jaji Kisanga
alifariki dunia jana Jumanne Januari 23,2018 katika Hospitali ya Regency jijini
Dar es Salaam.
Taarifa ya
Ikulu iliyotolewa leo Jumatano Januari 24,2018 imemkariri Dk Magufuli
akisema Jaji Kisanga atakumbukwa kwa mchango wake alioutoa kwa Taifa wakati
wote wa utumishi wake.
Dk Magufuli
amesema utumishi wa Jaji Kisanga ulijaa umakini, uchapakazi, uzalendo na
ushirikiano kwa wengine, mambo ambayo yalimwezesha kupata mafanikio makubwa.
Sote
tunafahamu kazi nzuri alizofanya akiwa katika majukumu ya kitaifa, mchango wake
katika kuijenga taaluma ya uanasheria baada ya uhuru na uanzishaji wa Mahakama
ya Rufani baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, kwa
hakika mchango wake hautasahaulika,” amesema.
Rais Magufuli
amemuomba Profesa Juma kufikisha rambirambi kwa familia ya Jaji Kisanga, majaji
na wanasheria wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.
Pia, amewaomba
wafiwa kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki
cha majonzi.
Rais Magufuli amlilia Jaji Kisanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment