Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini
(CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel
Masonga imeharishwa hadi kesho ambapo upande wa walalamikiwa wataanza kutoa
utetezi wao.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu
Mkazi wa Mkoa wa Mbeya Michael Mteite, baada ya kutupilia mbali pingamizi
lililowekwa siku ya jana na kuweza kusikiliza ushahidi huo wa sauti kwa
takribani dakika 39 uliyotolewa na shahidi namba tano wa kesi hiyo Afande
Joramu Magova ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama katika Ofisi ya Upelelezi
Mkoani humo.
Kutokana na hilo Wakili Mkuu wa Serikali Joseph
Pande, ameieleza Mahakama kuwa wameamua kufunga ushahidi upande wa Jamhuri
kwa kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na mashahidi wengine mara
baada ya kuridhika na shahidi namba tano wa Afande Joramu Magova, ambaye
alikuwepo kwenye mkutano na kurekodi sauti kwa kutumia kinasa sauti.
Hata hivyo Wakili wa utetezi ukiongozwa na Boniface Mwabukusi
akaiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi siku ya Alhamisi (kesho) saa nne
asubuhi kwa madai ya kuongea na wateja wake ambao wanatokea mahabusu na
kuongeza kuwa upande wa utetezi utakuwa na mashahidi saba na vielelezo
nane na kuiomba Mahakama shauri la mashtaka walipate pamoja na sauti za
watuhumiwa ili kujipanga na wateja wake.
Kwa upande mwingine katika kesi hiyo leo imeweza kusikilizwa na
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe.
Freeman A. Mbowe akiwa ameongoza na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mbeya
Sophia H. Mwakagenda ambapo nje ya Mahakama Mbowe aliwataka wanachama kuwa
wavumilivu wakati kesi hiyo ikiendelea.
Kesi ya Sugu yapigwa tena kalenda mpaka Alhamisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment