Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akitoa maelekezo katika kituo cha Afya
Mikumi baada ya kupokea Taarifa ya Ujenzi.
|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiendelea na Ukaguzi katika kituo cha Afya Mikumi
Wilayani Rombo.
|
Hii
ni baadhi ya muonekano wa majengo yanayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Mikumi-Rombo.
|
Muonekano
wa majengo yanayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Mikumi-Rombo.
|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akipokea
Taarifa ya Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kitoa cha Afya Karume kilichopo
Wilayani Rombo
|
Nteghenjwa
Hosseah, TAMISEMI.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ametoa mwezi mmoja
kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kukamilisha ujenzi wa kituo cha
Afya Karume ambao uko nyuma ya wakati kwa mujibu wa ratiba ya ujenzi wa vituo
hivyo ambao unaendelea kote Nchini.
Wakati akikagua Kituo
hicho Waziri Jafo amesikitishwa na kasi ndogo ya Ujenzi wa Kituo hicho
unaopelekea kuzorotesha malengo ya Serikali ambao umejikita katika Utoa.
Waziri Jafo alisema
Kituo hiki kimepokea Fedha za ujenzi tangu mwezi Septemba, 2017 na kilitakiwa
kiwe kimekamilisha ujenzi huu mwishoni mwa Disemba 2017, lakini mpaka
sasa ujenzi ndio umefikia kwenye hatua ya Kuezeka.
“Nataka mkajifunze kwa
wenzenu ambao walipokea Fedha za Ujenzi sawa na nyie na wamekwishajenga Nyumba
ya Mtumishi, Jengo la Maabara, Chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama, Chumba
cha kuhifadhia maiti, pamoja na kichomea Taka” Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa Kwenye
baadhi ya vituo vya Afya wamejitahidi kutumia kwa umakini Fedha hizo na
kuongeza na Njia ya Kutembelea Wagonjwa, wodi ya watoto na kufanya Ukarabati
majengo ya zamani kwa gharama hiyo hiyo ya Tsh Mil 500 ambazo nyie mpaka
sasa hamjakamilisha majengo yenu”
Alimalizia kuwa ifikapo
Tar. 25 Februari 2018 ujenzi wa miundombinu hii ya kituo cha Afya iwe
imekamilika na nipate Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na ikiwezekana nitapita
mwenyewe kuhakiki ubora wake.
WAZIRI JAFO ATOA MWEZI MMOJA UKAMILISHAJI WA KITUO CHA AFYA KARUME – ROMBO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment