Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anatafakari uwezekano wa kuanza tena kuwanyonga wahalifu nchini humo..
Rais amesema licha ya kwamba yeye ni “Mkristo” na dini yake
imemzuia kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wale ambao wamehukumiwa kunyongwa,
hata hivyo amesema, hali hiyo imekuwa ikiwatia moyo wahalifu.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kuhitimu
kwa askari wa idara ya magereza, katika gereza la Luzira jijini Kampala ambapo
ni miaka 13 sasa tangu Uganda ilipotekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu.
Watetezi wa haki za kibinadamu wameshutumu tamko hilo la Rais
Museveni na kusema adhabu ya kifo haikomeshi uhalifu.
Mara ya mwisho kwa Rais Museveni kuidhinisha hukumu ya kifo
itekelezwe ilikuwa katika gereza la Luzira mwaka 1999 na mwaka 2005
aliidhinisha mahakama ya kijeshi kutekeleza hukumu ya kifo
Rais airejea hukumu ya kunyongwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment