Ben
Komba/Pwani
Msimu mpya wa kilimo cha mpunga mwaka 2018/2019 umezinduliwa rasmi
katika halmashauri ya Chalinze, mkoa wa Pwani kuashiria kuanza rasmi kwa
shughuli za kilimo.
Akizindua msimu wa kilimo katika skimu ya umwagiliaji ya kilimo
cha Mpunga ushirika wa CHAURU, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO
amewataka wakulima katika mkoa huo kutumia kanuni za kilimo bora ili kupata
mafanikio wanayoyatarajia.
Aidha
amesisitiza kunyang’anywa mara moja heka 300 za ardhi zilizokuwa
zinashikiliwa na mwekezaji wa Kichina GUO MINTANG kama ilivyoagizwa na
aliyekuwa Naibu Waziri kilimo, uvuvi na mifugo, MH. WILLIAM OLE NASHA ili
zitumike kwa kilimo katika msimu huu wa kilimo.
Naye
Mwenyekiti wa Ushirika huo, BW.SADALLAH CHACHA akizungumzia juu ya maandalizi
waliyofanya katika msimu wa kilimo2018/2019 amesema wamejiandaa kikamilifu kwa
kuweza kununua trekta mpya moja aina ya NEW HOLLAND yenye horse power 90.
Ameongeza kuwa kwa upande wa pembejeo wamejipanga wao kama
wasimamizi wa ushirika huo kununua pembejeo hizo na kuwauzia wakulima katika
skimu hiyo.
MSIMU WA KILIMO 2018/2019 WAZINDULIWA RASMI PWANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment