Wakazi wa Karatu na baadhi
ya wabunge wamejitokeza kuaga mwili wa mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu,
Moshi Darabe (57).
Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii waliopo wilayani Karatu wameshiriki
shughuli hiyo leo Jumatano Januari 24,2018 wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati
hiyo, Kemilembe Luota.
Shughuli ya kuaga mwili imefanyika
katika viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu na mazishi yatafanyika katika
Kata ya Baray.
Wabunge kutoka CCM waliokuwepo ni
Nape Nnauye wa Mtama, Mary Chatanda (Korogwe) na Joseph Musukuma (Geita
Vijijini).
Kutoka Chadema wabunge waliokuwepo
ni Willy Qambalo wa Karatu, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki); Lucy Owenya na
Grace Kiwelu (Viti Maalumu).
Darabe aliyekuwa diwani wa Baray
alifariki dunia Jumapili Januari 21,2018.
Alikuwa mwenyekiti wa Chadema
wilayani Karatu tangu mwaka 2003 na alishika wadhifa wa udiwani kuanzia mwaka
2000
MWILI WA KIONGOZI WA CHADEMA WAAGWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment