Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu
Secilia, Kigango cha Muze Parokia ya Zimba, Jimbo Katoliki Sumbawanga, Flora
Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya
shukrani akiwa kanisani.
Tukio hilo lilitokea Jumapili
iliyopita saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza wakati kwaya ya
Mtakatifu Secilia ilipokuwa ikimsifu Mungu katika ibada hiyo.
Akizungumzia tukio hilo, mwalimu wa
kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Katekista Philipo Lupadasi alisema
wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani
alirejea katika sehemu yake kwenye kwaya na kuendelea kuimba lakini ghafla
alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha ibada kusimama kwa muda.
Alisema wanakwaya wenzake
walimnyanyua na kumtoa nje ya kanisa ili apate hewa wakiamini kuwa amepoteza
fahamu. Katekista huyo alisema baada ya kumpepea kwa muda, waliona hapati
fahamu hali iliyowalazimu kumpeleka Zahanati ya Kijiji cha Muze kwa ajili ya
matibabu.
Alisema baada ya kufikishwa katika
zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia uchunguzi
walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia.
Baada ya kupewa taarifa za kifo
hicho, wanakwaya hao waliangua kilio na hawakuweza kurudi tena kanisani kuimba
katika ibada ya pili na badala yake waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka
nyumbani kwake kwa taratibu za mazishi.
Mwalimu wa kwaya hiyo, Aloyce
Mwandanje alisema kuwa kifo cha mwanakwaya mwenzao ambaye alikuwa na ujauzito
wa miezi mitano, kimewaachia majonzi makubwa lakini hawana la kufanya kwa kuwa
ni mapenzi ya Mungu.
AFARIKI WAKATI AKITOA SADAKA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment