Takriban watu 27 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa karibu na msikiti
mmoja katika mji wa Benghaz nchini Libya utokana na shambulio la
kigaidi.Washambuliaji walitumia gari lenye vilipuzi kutekeleza mpango wao huo.
Milipuko hiyo miwili
nje ya msikitiki karibu na eneo la Al Suleiman,ilitokea jioni katika swala ya
maghari,ambapo waumini hao wakati wanatoka ndani ya msikiti ndipo walipolengwa
na shambulio hilo.
Vipande vya picha za
video zilizoonyeshwa kupitia Televishen ya taifa,zimeonesha miili ya watu waliouawa
katika shambulio hilo ikiwekwa ndani ya gari la Polisi.
Katika shambulizi hilo
gari la kwanza lilifika wakati waumini wakitoka na kulipuka,ambapo gari la pili
katika shambulizi hilo lililipuka muda mfupi upande wa pili wa mtaa huo dakika
chache baadaye lililo beba vilupuzi
Wanajeshi pamoja na
raia ni miongoni mwa watu waliathiriwa na shambulizi hilo.Hata hivyo idadi ya
watu waliojeruhiwa na vifo huenda ikapanda kutokana na watu wengi kujeruhiwa.
Bado haijafahamika
kwamba ni kundi gani lililoshiriki katika shambulizi,kwani hakuna ujumbe wowote
uliotolewa kukiri kushiriki.
Mji wa Benghazi
umekuwa kitovu cha machafuko kati ya wapiganaji na vikosi vya serikali.
Hata hivyo pamoja na
kwamba Libya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mambomu,lakini milipuko
miwili ndani ya dakika 15 ni jambo lisilo la kawaida
Taifa la Libya
lilijikuta katika machafuko Zaidi, baada ya kuangushwa kwa utawala wa Muamma
Gaddafi mwaka 2011,ambapo makundi yanayotaka kutwaa madaraka yakaibuka na hivyo
kutoka mwanya wa kundi la kigaidi la Islamic state kuimariki nchini humo.
Watu 27 wauawa katika mlipuko Libya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment