Kamati ya
Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeiagiza Serikali kupiga marufuku
matumizi ya mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi ili kulinusuru Taifa na
madhara yanayotokana na mifuko hiyo.
Maagizo hayo
yalitolewa baada ya kamati hiyo jana kukutana na Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Akizungumza
jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Sadiq Murad alisema walipata maelezo kutoka
serikalini kuwa uzalishaji katika viwanda 41 vya plastiki nchini ulikuwa ni
tani 73 katika mwaka 2016.
Hata hivyo,
alisema mifuko iliyoingia nchini kupitia bandarini na mipakani ilikuwa tani
1,375.
“Kamati
ilishauri ipigwe marufuku mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi na iwekwe
tahadhari katika mipaka yetu,” alisema.
Alisema kamati
inaitaka Serikali kufanya uhakiki wa uzalishaji katika viwanda vya nchini
ambavyo vimepunguza uzalishaji ili waweze kukaa chini na kuzalisha mifuko
ambayo itakayokidhi mahitaji na vigezo.
“Na hii
itakuwa ni ya muda kuzalisha mifuko hiyo kwa masharti ya vigezo baadaye
Tanzania isiwe na uzalishaji wa mifuko hii tena inayoharibu mazingira,”
alisema.
Murad alisema
zipo nchi nyingine kama Kenya, Rwanda, Uganda na Zanzibar ambazo zimepiga
marufuku uzalishaji na uingizaji wa mifuko hiyo na kutafuta mifuko mingine
inayotengenezwa na nguo, karatasi na majani.
Alisema mfano mzuri ni Zanzibar ambayo imepiga
marufuku mifuko hiyo tangu mwaka 2016 na mtu anapoingia na mifuko hiyo
bandarini hunyang’anywa na kupewa mingine.
Tueleweke
kabisa sisi kama kamati hatutaki kiwanda chochote kifungwe, tunataka uzalishaji
kwa kufuata masharti na vigezo. Tunaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za
kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda lakini vigezo na masharti lazima
yazingatiwe,” alisema.
Akizungumzia
agizo hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba
alisema hawaja japelekewa rasmi hayo mapendekezo. Hata hivyo alisema watapiga
marufuku mifuko yote ya ndani na nje. “Wenye viwanda wajiandae maana yake
dhamira ya Serikali wanaijua tangu mwaka 2016,” alisema
Kamati ya Bunge yatoa agizo Kuhusu mifuko ya plastiki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment