Mwalimu mmoja wa shule
ya wanafunzi wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,
amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa tuhuma za kufanya mapenzi na
mwanafunzi mwenye ulemavu na kumsababishia ujauzito.
Akizungumza katika
kongamano la wadau wa elimu lililoandaliwa na shirika la TCRS, Mkuu wa wilaya
Kilwa, Christopher Ngubiagai, amesema kitendo kilichofanywa na mwalimu huyo sio
cha kukifumbia macho huku mwanafunzi akiwa amekatisha kuendelea na masomo yake.
Mkuu huyo wa wilaya
pia, akaeleza wilaya yake inavyoathirika na tatizo la mimba za utotoni na utoro
na kupelekea kufanya vibaya katika mitihani ya Kimkoa na Kitaifa.
Wilaya hiyo imeshika
nafasi ya sita kati ya wilaya sita za mkoa wa Lindi katika matokeo ya mitihani
wa darasa la Saba mwaka jana, huku ikishika nafasi ya 160 Kitaifa.
Mwalimu mbaroni kwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye ulemavu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment