Waziri Mwigulu apiga stop utaoaji wa Passport

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo Januari 25, 2018 amesimamisha utoaji hati za kusafiria “Passport” za jumla na makundi kwa muda, kutokana na kupokea taarifa ya mateso wanayoyapata vijana wanaosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nje ya nchi kwa kisingizo cha kufanyakazi tofauti tofauti.

Waziri Mwigulu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Ofisi za Uhamiaji yaliyopo Kurasini Jijini Dar es salaam na kusema kuwa “Sisi kwenye Wizara yetu natoa tamko na kuelekeza kwamba nasimamisha utoaji wa hati ya kusafiri ‘Passport’ za jumla za makundi za vijana wanaokuwa wanapata mikasa hiyo ya kunyanyaswa, kutumikishwa, kuteswa kikatili na wengine kuwekwa rehani kwa masuala ya dawa za kulevya”, alisema Waziri Nchemba.

Pamoja na hayo, Waziri Nchemba aliendelea kwa kusema “tunasimamisha mpaka pale tutakapokuwa tumeweka utaratibu uliyokuwa rasmi na mzuri kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya nchi husika ambako kutakuwa na mahitaji ya aina hiyo. Mfano mzuri Kenya ilipokuwa inahitaji madaktari walitumia utaratibu uliyo rasmi kuomba madaktari hao. Kwa hiyo huo ndio utakaji wa kundi wa raia walio wengi kwa pamoja”.

Share this:

Waziri Mwigulu apiga stop utaoaji wa Passport Waziri Mwigulu apiga stop utaoaji wa Passport  Reviewed by KUSAGANEWS on January 25, 2018 Rating: 5

No comments: