Watu watano wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi
kuteketea kwa moto.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 25,2018
eneo la Mitondooni wilayani Magharibi B, Unguja.
Chanzo cha moto kinaelezwa kuwa ni hitilafu ya umeme ndani
ya nyumba waliyokuwa wakiishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali
amesema moto ulitokea saa moja usiku.
Mayasa Makame aliyenusurika katika janga hilo amesema moto
ulizuka ghafla walipokuwa wakipika.
Amesema wamepoteza kila kitu kilichokuwamo ndani.
Kuhusu chanzo cha moto imeelezwa huenda ikawa ni hitilafu ya
umeme kwenye jokofu.
Mayasa ameiomba Serikali na wananchi kwa jumla kuwasaidia
kwa kuwa hawana chochote kwa sasa.
Moto wateketeza nyumba ya makazi Nzazibar
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment