Maji yapatikane Shule ya Sekondari Kondoa - Jafo!


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Bweni katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikagua vyoo vya shule ya Wasichana Kondoa ambavyo viko katika hali mbaya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) alishiriki kifungua kinywa (Uji) katika Jiko la Shule ya wasichana Kondoa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikagua Chumvi inayotumika kupikia wanafunzi wa Kondoa kama ina madini Joto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Mchepuo wa Sayansi(PCM).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kupeleka Miundombinu ya Maji katika Shule ya Wasichana Kondoa Sekondari.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani humo na kukagua Majengo ya Sekondari Kondoa kabla ya Ukarabati Mkubwa unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Nimekuja leo katika Shule hii kwanza kukagua uchakavu wa majengo wanayotumia watoto wetu, kuzungumza na wanafunzi na kuskia kutoka kwa Mhandishi Mshauri kile wanachotarajia kufanya katika kazi ya ukarabati waliyopewa alisema Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa “Katika Ukaguzi wangu nimegundua uchakavu wa Mabweni, Ofisi za Walimu, Madarasa, bwalo, Jiko lakinI zaidi nimegundua uchakavu wa vyoo  na ukosefu wa maji  katika Shule hii”

Aliongeza kuwa Uchakavu wa vyoo kwa namna hii ni hatari kwa maisha ya wanafunzi wetu , na wakati wowote unaweza kusababisha matatizo na huu ukosefu wa maji ndio unazidi kuvifanya vyoo hivi kuwa hatari Kiafya na kuonekana vichafu zaidi nasisitiza katika Ukarabati unaoaza Muanze na vyoo na vijengwe upya na wala sio kukaraati hivi vya zamani.

Maji ni kitu muhimu sana katika shughuli zetu za kila siku na katika suala la usafi maji ni muhimu sana na wanafunzi hawa wako zaidi ya mia tano kwahiyo kukosekana kwa Maji kunasabisha uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha Afya zao, hivyo Mkurugenzi nataka nikirudi hapa Mwezi wa Tano nikute maji yanatoka, vyoo vipya sambama na Ukarabati ulioanishwa, alimalizia Jafo.

Katika kikao chacke na wanafunzi wa shule hiyo wanafunzi wa Shule hiyo walimuahidi Waziri jafo  matokeo mazuri katika mtihani wa kidato cha sita utakaofanyika mwaka huu na kusema kuwa watafanya vizuri na alama za mwisho kwa mwanafunzi zitakuwa daraja la II.








Maji yapatikane Shule ya Sekondari Kondoa - Jafo! Maji yapatikane Shule ya Sekondari Kondoa - Jafo! Reviewed by KUSAGANEWS on January 25, 2018 Rating: 5

No comments: