Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite amekataa kujitoa kusikiliza kesi
inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na mwenzake.
Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha
ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli wanayodaiwa kuitoa Desemba 30,2017.
Awali, leo Alhamisi Januari 25,2018
Sugu na Masonga waliwasilisha ombi mahakamani wakimkataa hakimu huyo wakitaka
ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye.
Hakimu Mteite amesema sababu
zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria na hazimfanyi kujitoa.
Baada ya hakimu kukataa kujitoa,
mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha
washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo.
Sugu, mwenzake wamkataa hakimu Sugu
na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta mawakili
wengine.
Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi
Februari 2,2018 na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.
Hakimu akataa kujitoa kwenye Kesi ya Sugu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment