Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi amezitaka wizara, taasisi za Serikali na vyombo vyote
vya umma kupima maeneo yao na kuyawekea alama za mipaka kuepusha uvamizi.
Lukuvi amesema hayo baada ya kukagua maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Akiambata na naibu wake, Angelina Mabula ambaye ni mbunge wa Ilemela, Lukuvi ametembelea maeneo yaliyovamiwa na wananchi ya Polisi Kigoto-Kirumba, Uwanja wa Ndege wa Mwanza na eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) la Nyamirolerwa
Katika taarifa ya wizara iliyotolewa leo
Jumapili Januari 28,2018 Lukuvi amezitaka taasisi zote za Serikali kupima
maeneo yao ili wananchi wayatambue.
Amewataka waliojenga ndani ya hifadhi ya
Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuondoa maendelezo yao ndani ya siku saba kabla ya
kuchukuliwa hatua.
Lukuvi amesema hawaruhusiwi kukaa karibu na eneo linalorusha na kutua vyombo vya anga jambo ambalo ni hatari kwao na usalama wa vyombo hivyo.
Pia, amezitaka halmashauri zote nchini kukamilisha ukusanyaji wa kodi ya ardhi kabla ya Aprili 30.
Ametoa agizo hilo baada ya kukutana na
watumishi na wakuu wa idara wa Manispaa ya Ilemela na wa Jiji la Mwanza baada
ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la ardhi na maendeleo ya
urasimishaji makazi mkoani Mwanza.
Lukuvi Ataka maeneo Kupimwa ili kuepusha migogoro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment