Mwenyekiti wa CHADEMA
Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kulaani vikali kitendo alichofanya Waziri wa
Mambo ya ndani pamoja na Waziri wa TAMISEMI kumpigia kampeni mgombea wa Ubunge
wa CCM jimbo la Siha na kusema kauli zao zimejaa ubaguzi wa wazi wazi.
Mbowe amesema wakati
akizindua kampeni za wagombea wa Ubunge na udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika
jimbo la Siha na kudai Mawaziri hao wamekuwa wakitumia vibaya madaraka
yao.
"Kaja Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anawaambia
kuwa lazima mchague CCM, anakuja Jafo Waziri wa TAMISEMI anawaambia wananchi wa
Siha ili mpate maendeleo labda mumchague Mollel, huu ni ujinga mtupu.
Tunapoongozwa na viongozi wa sampuli hizi, viongozi wabaguzi, viongozi waliopewa
dhamana ya maisha yetu wakafikiri ni mali za baba zao na mama zao wanakuja
kutuambia upumbavu watu wa Siha tunaakili, kujengwa kwa barabara si fadhila ya
Rais" alisema Mbowe
Mbali na hilo Mbowe alisema kuwa katika uchaguzi huu wa sasa
endapo wataona gari za Serikali zikitumika kwenye kampeni za wagombea wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) zitakuwa halali yao.
"Mzee Mwambigija safari hii kama kufa tufe, safari hii kama
noma na iwe noma tunaomba magari ya Serikali yatumike kwa kazi za Serikali
hatutakuwa na ugomvi lakini magari ya Serikali na vyombo vya Serikali
vikitumika kwenye kampeni za chama chochote ni halali yetu, kwa sababu nchi hii
inaonekana siasa za kistaraabu haziwezekani" alisisitiza
Mbowe
"Huu ni ujinga mtupu" - Freeman Mbowe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment