Mbowe Siha "Dokta Mollel hajazuiliwa na mtu Kuongea bali ni Dkt asiye na uwezo,

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kukanusha taarifa alizotoa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Siha, Dkt Mollel kuwa aliamua kuhama CHADEMA na kwenda CCM kwa kuwa alizuiwa kuongea na viongozi wa CHADEMA.

Mbowe amesema hayo leo katika uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Siha, Elvis Mosi na kudai kuwa Moller hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na ni mtu ambaye amekuwa akijikomba kwa watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  

"Mollel hajazuiliwa na mtu bali ni Dk. asiye na uwezo, hana uwezo wa kujenga hoja ni mwanaume anajikomba komba kwa watu wa CCM, niwambie watu wangu wa Siha mnapokuwa mnachagua viongozi sisi kama chama tunawapima kila mwaka, huyu uchaguzi unaokuja atarurudishia jimbo au atatunyima jimbo? Na kwa vigezo mbalimbali vya chama vilivyofanyika wananchi wa Siha mshukuru kwa sababu mlikuwa unatuchagulia gunia la misumari bila kujua, angebaki kwa miaka mingine mitatu kwenye nafasi yake ya Ubunge CHADEMA wananchi wa Siha mngeichukia" alisema Mbowe 

Mbowe aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha Mollel kujivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge jimbo la Siha ni mpango wa Mungu na ni jambo zuri kwani lingefanya chama hicho kuchukiwa na wananchi. 

"Huu ni mpango wa Mungu aliona wananchi wa Siha nikiwaachia hili gunia la misumari litakuwa si jambo zuri hivyo akamtia uchizi akaamua kuhama chama, kwa hiyo hatuna cha kulia kila kitu ni mpango wa Mungu, alijua kwamba Siha tumejitwisha gunia la misumari" 


Mbowe Siha "Dokta Mollel hajazuiliwa na mtu Kuongea bali ni Dkt asiye na uwezo, Mbowe Siha "Dokta Mollel hajazuiliwa na mtu Kuongea  bali ni Dkt  asiye na uwezo, Reviewed by KUSAGANEWS on January 26, 2018 Rating: 5

No comments: