Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani
Songwe, John Palingo ameamuru kuwekwa mahabusu mkandarasi wa umeme kutoka
Kampuni ya Cyber, Benjamin John baada ya kutuhumiwa kuchukua fedha kwa
wananchi kwa madai ya kuwaunganishia umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini
(Rea) katika vijiji ambavyo havipo kwenye mpango huo
Palingo alitoa amri hiyo jana
kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbozi baada ya baadhi
ya madiwani kudai kampuni hiyo imekuwa ikiwatoza baadhi ya wananchi Sh20,000
hadi 140,000 kwa ajili ya fomu na usajili wa mteja kuunganishiwa umeme.
Kutokana na malalamiko hayo
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Ambakisye alilazimika kuuita uongozi wa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Songwe na mwakilishi wa Kampuni
ya Cyber kutoa ufafanuzi mbele ya baraza hilo.
Hata hivyo, Mkandarasi na
mwakilishi wa Kampuni ya Cyber, Benjamini John alipotakiwa kutoa ufafanuzi
alikanusha madai hayo akieleza kwamba iwapo itathibitika kuwa kampuni yake
imehusika, fedha hizo zitarejeshwa kwa waliotapeliwa.
Hizi ni tuhuma, naamini vyombo vya
dola vitachunguza na mwisho wa siku ukweli utabainika, hata hivyo kampuni hii
imesajiliwa kihalali lakini pia kutokana na ushindani wa kibiashara
inawezekana miongoni mwa madiwani ni washindani wetu wametuingiza katika
kashifa hii,” alisema John.
Akitoa uamuzi wake, Mkuu wa wilaya
hiyo Palingo aliamuru polisi kumshikilia mkandarasi huyo kwa ajili ya
uchunguzi na kuwataka madiwani kwa upande wao kuwasilisha ushahidi wa tuhuma
wanazodai ofisini kwake ifikapo Jumatatu ili hatua zaidi zichukuliwe
|
|
DC Palingo aamuru mkandarasi akamatwe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment