Naibu Waziri wa Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto , Dk Hamisi Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakikisha wanaboresha huduma za Afya katika Wilaya hiyo hasa katika kituo cha Afya Mkasale.
Kituo hicho kimebainika kuwa na huduma mbovu, kikiwa na majengoi chakavu hali ambayo inahatarisha usalama na afya za watumishi na wagonjwa wanaofika kupata huduma.
Dk Kigwangala alikuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa utekelezaji wa agizo la uboreshaji wa vituo vya afya kila Kata nchini lilitolewa Desemba 2016.
Akikagua kituo hicho cha Mkasale, Dk Kigwangallah aliona mazingira yasiyoiridhisha na mara moja akauagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kushughulikia changamoto hiyo ndani ya miezi mitatu.
Alimtaka mhandisi wa maji kuhakikisha kituo hicho kinapatiwa huduma hiyo.
“Nautaka uongozi wa kijiji kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka kituo hiki,” alisema na kuongeza;
“Hata hivyo nawasihi wananchi tumuunge mkono Raisi John Pombe Magufuli kwa vita aliyoianzisha ya kulinda rasilimali za nchi yetu kwani taifa limekuwa likiibiwa kwa muda mrefu sana ila umefika muda kuhakikisha kuwa rasimali za nchi zinatunzwa na kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.”
Aliendelea kusema kuwa ili mwananchi aweze kushiriki katika shughuli za uzalishaji ni lazima awe na afya njema na ili awe na afya njema ni lazima wananchi kwa kushirikiana na serikali kuboresha vituo vya kutoa huduma za afya na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
No comments:
Post a Comment