Mawaziri wawili wa Kenya walazwa hospitalini na dalili za kipindupindu



Mawaziri wawili nchini Kenya ni miongoni mwa watu kadhaa waliolazwa hospitalini wakiwa na dalili za kipindupindu. 

Waziri wa fedha Henry Rotich na wa viwanda Adan Mohamed waliugua baada ya kuhudhuria mkutano wa maonyesho ya kibiashara katika jumba la kimataifa la mikutano la Kenyatta KICC mjini Nairobi mapema wiki hii. 

Takriban washiriki wengine 70 wa mkutano huo pia wamelazwa katika hospitali mbali mbali mjini Nairobi wakiwa na dalili hizo za ugonjwa wa kipindupindu. 

Mkurugenzi wa idara ya huduma za afya katika wizara ya afya Jack Kioko amesema maafisa wanachunguza iwapo mawaziri hao na wageni wengine waliohudhuria mkutano huo wana kipindupindu au walikula chakula ambacho kilikuwa kimeharibika. 

Mwezi uliopita, madaktari na wahudumu wa afya takriban 50 waliokuwa wakihudhuria kongamano la kimataifa katika hoteli moja ya kifahari Nairobi pia walilazwa baada ya kupatikana na kipindupindu.
 Chanzo :DW


Mawaziri wawili wa Kenya walazwa hospitalini na dalili za kipindupindu Mawaziri wawili wa Kenya walazwa hospitalini na dalili za kipindupindu Reviewed by KUSAGANEWS on July 15, 2017 Rating: 5

No comments: